Tuesday, February 28, 2012

SHUHUDIA UJIO WA KIPINDI KIPYA CHA TV "ONGEA NA JANET TV TALK SHOW"!

                     Janet akiwa na mdau wake wakifurahi mara baada ya kumaliza kurekodi kipindi.
Mtayarishaji wa kipindi cha Ongea na Janet TV talk show pichani kulia akiwa na mmoja wa mwanasumbwi hapa nchini Japhet Kaseba akifanya nae mahojiano kwenye moja ya kipindi chake.
Mtayarishaji wa kipindi cha Ongea na Janet TV talk show pichani kulia akiwa na mmoja wa wadau akifanya nae mahojiano kwenye moja ya kipindi chake.

Na Mwandishi Wetu

Ongea na Janet ni Talk show ambayo inazungumzia mambo yanayotugusa katika maisha yetu ya kila siku, Inahusisha Jinsia zote na rika zote. Kipindi changu nilikitengeneza mwaka 2009 june 26 lakini bahati mbaya ilikuwa ni ngumu sana kupata airtime hasa ikizingatiwa ni kipindi toka nje ya kampuni husika,bado wahusika hawajakubali kubadilika ila hii "ishu" digital itasaidia sana. -Sijaajiriwa na Clouds Tv bali tumeingia Mkataba kama partiners .


Ni kipindi ambacho sitegemei kishuke bali kitakuwa kinapanda na watu wategemee mabadiliko,nimeanzia chini napanda juu katika kuleta changamoto,Natamani watu wenye talents wazitumie bila kuogopa na wasikate tamaa,kwa mfano,nimehangaika na kipindi changu kwa miaka mitatu na sasa ndio naanza kuona matunda ya uvumilivu,ubishi wa kutimiza ndoto na kutokukubali kushindwa kufikia malengo.


Wasijali maneno ya watu ya kukatisha tamaa,mtu asimame kwenye anachokiamini na akifanyie kazi haijalishi itachukua muda gani.Nategemea,kuelimisha,kushauri na kuburudisha. Niliacha kazi ITV 2008,then nika-join NGO from Canada lakini damu yangu iko kwenye media...nimeamua kurudi na kuacha kila kitu nyuma. Nataka kukamilisha ndoto zangu zote zilizosimama kwa miaka 4. Kipindi kinaanza tarehe 8 March,alhamis saa 3 kamili. Shukrani kwa Jiachie Blog!

No comments:

Post a Comment