Tuesday, February 28, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UMWAGIALIAJI KISEGESE-RUNGWE


Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mtaro wa kupitishia maji ya umwagiliaji katika Kilimo mradi uliopo katika Kijiji cha Kisegese, wakati akiwa katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana Februari 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi katika chanzo cha mradi wa maji ya umwagiliaji katika Kijijji cha Kisegese, Wilaya ya Rungwe mtaro wenye urefu wa Kilomita 7, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya  Februari 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, wakiangalia Mpunga katika eneo la Shamba Darasa, lililopo Kijiji cha Kisegese Wilaya ya Rungwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya, Februari 26, 2012.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATAWAZWA KUWA MZEE WA KABILA LA WANYAKUSA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Mkuki kutoka kwa mwakilishi wa Wazee wa Kabila la Wanyakyusa wa Kijiji cha Mbambo Wilaya ya Rungwe, Ambakisye Mwakatobe, ikiwa ni ishara ya kumkabidhi wadhfa wa kuwa Mzee wa Kabila la Wanyakyusa, wakati alipofika katika Kijiji hicho kuwahutubia akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana Februari 26, 2012. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment