Thursday, May 3, 2012

MUKAMA AKUTANA NA BALOZI WA NIGERIA, GRAND MALT PROMO, SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kulia) akizungumza na Balozi wa Nigeria hapa nchini, Ishaya Samaila Majanbu, Ofisini kwake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kulia) akiagana na Balozi wa Nigeria hapa nchini, Ishaya Samaila Majanbu, baada ya kuwa na mazungumzo, Ofisini kwake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.


 Kiwanji cha Grand Malt kisicho na kilevi leo kimezindua tuzo za 'Exel with Grand Malt"  kwa wanafunzi wa elimu ya juu ikiwa ni mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa ambapo jumla ya sh. milioni tano zimetengwa kuwazawadia watakaoshinda. Pichani, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) inayotengeneza kinywaji hicho, Fimbo Butala akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana kuhusu promosheni hiyo. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi.

Wakati jana ilikuwa siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, inaelekea mahitaji ya kusoma magazeti yapo kwa watu wa rika mbalimbali wakiwemo watoto. Pichani, watoto wakisoma magazeti kwa muuzaji, eneo la Kivukoni Front, Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo.

No comments:

Post a Comment