Sunday, February 19, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MITAMBO YA KUZALISHA UMEME WILAYA YA MBINGA!


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya kumbukumbu na Msanii Ofisa Utamaduni Mstaafu wa Wilaya ya mbinga, Benedict Maundi, baada ya kuzindua rasmi mitambo ya kuzalisha umeme na kuwahutubia wananchi wa Wilaya ya Mbinga akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Ruvuma, leo Februari 16, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kitufye ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi mashine za kuzzalisha umeme, wakati alipotembelea katika mradi huo uliopo Wilayani Mbinga akiwa katika ziara yake ya moa wa Ruvuma, jana februari 16, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tanesco, Eng. Boniface Njombe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika mradi wa mashine za kuzalisha umeme Wilayani Mbinga, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Ruvuma jana, februari 16, 2012.
Msanii Ofisa Utamaduni Mstaafu wa Wilaya ya mbinga, Benedict Maundi, akifurahia huku akipiga 'Vuvuzela la asili' wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alikuwa akiwasili kuzindua mashine za kuzalisha umeme Wilaya ya Mbinga jana Februari 16, 2012. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment