Sunday, February 19, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YA MKOA WA RUVUMA ATUA MKOA WA KATAVI LEO!


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Katoliki (W) Mbinga, John Ndimbo, wakati alipofika katika Kanisa Kuu la Katoliki Mtakatifu Kiliani, kwa ajili ya kufanya majumuisho baada ya kumazliza ziara yake ya mkoa huo jana Februari 17, 2012.
              MAKAMU WA RAIS ATUA MKOA WA KATAVI LEO KUANZA ZIARA YAKE.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Katavi Mkoa wa katavi kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku tatu ya mkoa huo leo Februari 18, 2012. Kushoto ni Mkewe Mama Asha Bilal, na (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya Mkoa wa Rukwa, wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Katavi mkoani humo leo Februari 18, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment