Hili ni eneo la Oldupai Gorge kama linavyoonekana kwa mbali. Kihistoria ndipo palipovumbuliwa fuvu la binadamu wa Kale Zinjanthropus Boisei.
Hii ilikuwa kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya utalii duniani Septemba 27 mwaka 2009 kwenye nuwanja wa Samora mkoani Iringa.
Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akishow luv na mmoja ya wazee wa jadi pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Phillemon Luhanjo.
Na Theeastaafrica Bloger
Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka. Lengo lake ni kuhamasisha na kuweka uelewa kati ya jamii za Kimataifa kuhusu umuhimu wa utalii na thamani yake kijamii, kisiasa, kitamaduni, na kiuchumi. Tukio hili hutafuta njia ya kukubaliana na changamoto zilizoorodheshwa katika malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa pamoja na kusisitiza mchango wa sekta ya utalii katika kuyafikia haya malengo.
Maadhimisho haya yatatoa fursa ya majadiliano kwa wadau wa sekta ya utalii yatakayo lenga katika kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya watoa huduma na bidhaa katika sekta ikiwa ni pamoja na wazalishaji wa vyakula na mahoteli. Hivyo, pamoja na maonesho haya, kamati ya maandalizi imeendaa mdahalo maalum utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Oktoba, 2011 kwenye ukumbi wa Karimjee.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Tourism-Linking Cultures Utalii unaunganisha tamaduni. Kauli mbiu hii inalenga katika kuhimiza mchango na umuhimu wa utamaduni katika utalii ili kuboresha maisha ya watu na kutoa fursa za jamii kufurahia urithi wa nchi zao na Dunia kwa ujumla. Ikumbukwe kwamba, utamaduni wetu ni sehemu ya Utalii wetu unaotuonesha tulikotoka, tuliko na tunakoelekea.
Aidha, ningependa kutumia fursa hii kuwaomba watanzania waupigie kura Mlima Kilimanjaro uweze kuwa moja kati ya maajabu saba ya dunia ambapo Tanzania inashindana na Table Mountain (South Africa).
Hadi hivi sasa muitikio wa wananchi kuupigia kura mlima wetu nimdogo ukilinganishwa na jinsi Afrika Kusini wanavyochangamkia kuupigia kura mlima wao ambao kimsingi hauna sifa zakuuzidi Mlima Kilimanjaro hivyo watanzania tubadirike na kuanza kuupigia kura mlima wetu.
No comments:
Post a Comment