Wednesday, January 4, 2012

SIKU RAIS JAKAYA AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WAWILI NA NAIBU KATIBU MKUU MMOJA IKULU DAR!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Paul, Katibu Mkuu Ikulu, Peter Alanambula Ilomo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Chacha, kabla ya kuapishwa wakati Makamu akiingia katika Ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa makatibu hao walipokuwa wakisubiri kuapishwa rasmi kushika nafasi hizo Ikulu Dar es Salaam leo Januari 2, 2012.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi, Nyaraka za Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Chacha, baada ya kumuapisha rasmi kushina nafasi hiyo, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Januari 2, 2012.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha, Susan Paul, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ikulu, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha makatibu wawili na Naibu Katibu mmoja, iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo Januari 2, 2012. 
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na Naibu Katibu Mkuu, walioapishwa leo Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa leo Januari 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment