Wednesday, January 4, 2012

RAIS KIKWETE ALIPOOMBOLEZA VIFO VYA AZIZ SHEWEEN NA BALOZI ATHUMANI MHINA!

Rais jakaya kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Aziz Sheween, Mikocheni jijini Dar es salaam, Jumatatu jioni nyumbani kwa Afisa huyo wa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, kilichotokea huko Riyadh, Saudi Arabia.
Rais Kikwete akiwa na familia na waombolezaji nyumbani kwa marehemu Aziz Sheween, Afisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefariki huko Riyadh, Saudi Arabia.
Rais Kikwete akiagana na familia ya marehemu ya Aziz Sheween, Afisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefairiki juzi huko Riyadh, Saudi Arabia.
                                Makada wa CCM wakiwa msibani kwa marehemu Balozi Mhina.

Rais Kikwete akipata maelezo alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana kuamkia jana alipokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.
   Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina enzi za uhai wake.

Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Khamis Dadi alisema Balozi Mhina alifariki usiku wa kuamkia jana aliokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.
Dadi alisema Mhina alikuwa akipelekwa hospitali baada ya hali yake kubadilika ghafla kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.Alisema mwili wa marehemu, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kwamba mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho.

No comments:

Post a Comment