Wednesday, January 18, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU REGIA MTEMA KARIMJEE DSM, KUZIKWA KESHO IFAKARA!


Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakiagana na wanafamilia ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Regia leo januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Tundu Lissu, Vita Kawawa, pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment