Wednesday, July 20, 2011

AJALI ZA BARABARANI ZAPOTEZA MAISHA YA WATU 1,700 NCHINI!


                                                ACP - JOHANSEN KAHATANO
Jeshi la Polisi nchini Kikosi cha Usalama Barabarani, limebainisha kuwa katika kipindi cha Miezi sita ya kwanza kwa mwaka huu zaidi ya watu elfu moja na mia saba wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali zinazotokea barabarani.

Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, ACP - JOHANSEN KAHATANO, amesema kwa upande wa pikipiki zikiwa zimeripotiwa ajali 2,856 ambazo zimesababisha vifo vya watu 396 ndani ya kipindi hicho.


Katika hatua Nyingine ACP - KAHATANO, amesema maadhimisho ya mwaka huu ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa yatafanyika Kagera na kuambatana na kauli mbiu inayosema Usalama Brabarani unahitaji juhudi za kila mmoja wetu.

No comments:

Post a Comment