Meneja wa benki ya KCB Tanzania Tawi la Arusha Bi Judith Lubuva akimkabidhi mwanafunzi wa shule Nakido ya jijini humo moja ya dawati kati ya 25 yaliyotolewa kama msaada wenye jumla ya shilingi Milioni 2/- wakati wa hafla iliyofanyika hivi karibuni. Wanaoshudia ni wanafunzi wengine wa shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Nakido ya jijini Arusha wakibeba madawati kati ya 25 yenye jumla ya shilingi Milioni 2/- yaliyotolewa na benki ya KCB Tanzania kama msaada kwa shule hiyo wakati wa hafla iliyofanyika hivi karibuni.
Meneja wa benki ya KCB Tanzania Tawi la Arusha Bi Judith Lubuva akiteta jambo na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Nakido ya jijini humo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 25 yaliyotolewa kama msaada kwa shule hiyo na kugharimu jumla ya shilingi Milioni 2/-.
Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Moshi Vijijini Bw Gerald Matemu akionesha baadhi ya vitabu kati ya 282 vilivyokadhiwa kwa shule ya msingi Sango kama msaada na Benki ya KCB Tanzania na kugharimu shilingi Milioni 2/- hafla iliyofanyika hivi karibuni. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Shule hiyo, Stella Maeda.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya msingi Sango Doren Duwaza moja ya vitabu kati ya 282 vilivyokadhiwa kwa shule hiyo kama msaada na kugharimu shilingi Milioni 2/- hafla iliyofanyika hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya msingi Sango John Chaki moja ya vitabu kati ya 282 vilivyokadhiwa kwa shule hiyo kama msaada na kugharimu shilingi Milioni 2/- hafla iliyofanyika hivi karibuni.
Na MwanaEastafrica, Arusha
Benki ya KCB Tanzania imekabidhi msaada wa vitabu na madawati vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 4/- kwa shule za msingi Sango ya Moshi, Kilimanjaro na Nakido ya jijini Arusha ili kuadhimisha wiki ya jamii kanda ya kaskazini.
Shule ya Msingi Sango iliyoko Moshi vijijini ilipatiwa msaada wa vitabu 282 vyenye thamani ya shilingi milioni 2 wakati ile ya Nakido iliyopo Arusha ilisaidiwa madawati 25 yaliyogharimu shilingi milioni 2/- pia. Akikabidhi msaada wa madawati kwa shule ya Nakido, Meneja wa KCB Tanzania tawi la Arusha Bi Judith Lubuva amesema msaada huo utakaotumika kwa ajili ya wanafunzi utawawezesha kuzingatia masomo wawapo darasani.
Kwa upande wake Meneja wa KCB Tanzania tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau aliomba jamii kuvitunza na kuvienzi vitabu wanavyotoa ili kutekeleza malengo ya millennia yanayozitaka nchi wanachama kuhakikisha kiwango cha elimu ya lazima kinafikia ngazi ya chuo kikuu hadi kufikia mwaka 2015. “Umasikini unachangia nchi zinazoendelea kama Tanzania kutekeleza kwa kusuasua mipango ya millennia katika sekta za afya, elimu na mazingira. Hivyo kwa kuvitunza vitabu hivi jamii itafaidika angalau kwa kupata elimu bora kuendana na soko la ajira Afrika Mashariki,” alisema Saitabau.
Kaimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sango Stella Maeda amesema msaada huo umekuwa changamoto kwao kwani utasaidia kuinua kiwango cha ufundishaji shuleni hapo tofauti na awali ambapo ilikuwa vigumu wanafunzi kushiriki kwa ufasaha. Akifafanua Mwalimu Maeda amesema awali walikuwa wakifundisha kwa uwiano kitabu kimoja kwa watoto wanne lakini msaada huo wa vitabu vitawezesha kila wanafunzi wawili kutumia kitabu kimoja jambo litakalosaidia kuongeza kiwango cha ufaulu.
“Tunashukuru msaada huu umekuwa changamoto, vitabu hivi vitatuwezesha kuongeza kiwango cha ufaulu kwani walimu pia kwa kutumia taaluma yao wataweza kuboresha kiwango cha elim,u shuleni hapa,” alisema Mwalimu Maeda. Mwanafunzi wa shule ya Msingi Nakido Rahma Mwinyi ameshukuru kwa msaada huo na kusema kitendo cha wanafunzi kukaa chini kinaathiri masomo na hivyo wataweza kuongeza kiwango cha mahudhurio darasani.
No comments:
Post a Comment