Friday, December 9, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, MGENI RASMI, MKESHA WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU MNAZI MMOJA DAR!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 8 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
                             Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.

Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba kupitia Chama cha Wananchi CUF, Hamad Rashid, akijumuika na vijana wa CCM pamoja na Ole Sendeka kucheza miondoko ya Taarab, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

No comments:

Post a Comment