Wednesday, December 21, 2011

POLISI YAWAKAMATA MADKTARI WA KUJITOLEA UWANJA WA TAHRIR!

Madaktari na wasaidizi wakujitolea, wamefungua vituo vya kutoa matibabu ya dharura kwenye uwanja wa Tahrir katikati ya mji mkuu wa Misri, Cairo kama ilivyokuwa wakati wa mapinduzi ya nchi hiyo mapema mwaka huu.

Watu wanaojeruhiwa katika machafuko yaliyozuka upya, wanahudumiwa katika zahanati hizo za dharura jambo ambalo linawakera wanajeshi.


AMANI MASSOUD ambaye ni mwanaharakati anayefanya kazi kwenye Shirika la Haki za Binadamu nchini Misri amesema madaktari wanaosaidia kwenye uwanja wa Tahrir huandika kila kitu kinachotokea huko kwa ajili yak kumbukumbu.


Hata hivyo ripoti zinazotolewa na madaktari na mashuhuda, zinatofautiana kabisa na taarifa zinazotolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo.Kwani hadi Jumanne mchana, Wizara hiyo iliripoti majeruhi kadhaa na wakati daktari mmoja kutoka uwanja wa Tahrir siku hiyo hiyo, aliripoti kuwa tangu mapema asubuhi, zahanati ilipokea maiti nne.

No comments:

Post a Comment