Tuesday, December 20, 2011

MVUA DAR ZALETA MAAFA NA KUUA WATATU DAR!

                                          Hili ni moja ya eneo lililokumbwa na mefuriko hayo.
Nyumba zikiwa zimezingirwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam leo.
Mmoja ya wakazi akipima maji ili kuona uwezekano wa kwenda kuwasaidia watu waliozingirwa na maji.
Baadhi ya wakazi wakiwa sintofahamu baada ya kushuhudia mafuriko yaliochokuwa maisha ya wapendwa watatu.
   Baadhi ya waokoaji wakiwa na vifaa vya kazi tayari kuokoa maisha ya wakazi wa mabondeni.

Na Mwandishi Wetu
Mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo zimesababisha maafa makubwa na watu watatu wamethibitishwa kupoteza maisha wakati baadhi ya familia zikikosa makazi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, ASP SULEIMAN KOVA, amewataja watu waliofariki dunia katika mvua hizo kuwa ni mwanamke mmoja GATI MAKA, mkazi wa Kitunda, ambaye alipigwa na radi eneo la Kurasini shimo la Udongo, MAGANGA SAID na IBRAHIM MSAME ambaye alifariki dunia baada ya kusombwa na maji na mwili wake kukutwa kwenye bonde la Msewe


Katika hatua nyingine, Wakazi wa Kigogo Mbuyuni, Kawe pamoja na Tandale kwa Mtogole wamelazimika kupanda kwenye paa za nyumba pamoja na minazi mirefu kunusuru maisha yao mpaka walipookolewa huku wengine wakibeba mali zao zilizosalimika katika mafuriko ya maji yaliyosababishwa na mvua hizo. Asante Michuzi JR kwa msaada wa picha!

No comments:

Post a Comment