Wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari nchini wameaswa kuwa makini wakati wa kufanya mchakato wa kutafuta vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi ili kuepuka kutapeliwa na kutozwa gharama kubwa zisizo na msingi.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya GLOBAL EDUCATION LINK inayojishughulisha na uwakala wa kusafirisha wanafunzi nje ya nchi ABDULKALIM MOLLEL, wakati wa wa kongamano maalum la kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania bara likiwashilikisha wakuu na wawakilishi wa vyuo vikuu mbalimbali kutoka nchi za India Ukrane, uingereza, na Malaysia.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika kongamano hilo wameziomba taasisi za vyuo vikuu hivyo kuhakikisha zinajenga vyou vikuu vya kimataifa hapa nchini ili kuhakikisha wanafunzi wa hali zote wanapata elimu ya juu.
No comments:
Post a Comment