Afisa Habari wa UN Information Centre (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwakaribisha wageni waalikwa katika semina ya mafunzo kwa vijana juu ya matumizi ya mtandao katika kuhamasisha haki za Binadamu iliyofanyika katika Ofisi za UN Information Centre. Human Rights Learning Program for Youth on Use of Social Media to Advocate For Human Rights imeandaliwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kwa Kushirikiana na Taasisi ya Under the Same Sun.
Afisa Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuhusiana na Azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwaka 1948 lenye vipengele 30 ambavyo vimeainisha Haki Msingi za Binadamu na Uhuru.
Mtaalamu wa IT na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Bw.Wilfred Warioba akielezea jinsi mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano kama vile Facebook, Twitter na Blogs zinavyofanyakazi na zinavyoweza kutumika kupashana Habari na Kuelimishana ambapo pia amesema iwapo itatumika vibaya inaweza kuelta madhara makubwa kwa watumiaji. Katikati ni Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG Bw. Ayoub Rioba na Afisa Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo.
Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Vicky Ntetema kutoka Taasisi inayotetea haki za jamii ya watu wenye Ulemavu wa Ngozi ya Under the Same Sun akieleza jinsi watu wengine wanavyoweza kutumia mitandao hiyo kukiuka haki za msingi za Binadamu kwa namna mbalimbali na kuwataka vijana kuwa makini na kuepuka kupeana ahadi za kukutana na watu wasiowajua waliowasiliana nao kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Blogs. Pamoja na mambo mengine Ntetema amewaasa vijana hao pamoja na jamii nzima kwa ujumla kutowaita watu kutokana na ulemavu walionao bali watumie majina yao halisi akitolea mfano kuwaita watu wenye ulemavu wa ngozi "Zeruzeru" (Albino).
Pichani Juu na Chini ni Wanafunzi na wageni waalikwa waliohudhuria mafunzo hayo wakitazama filamu "White and Blacks: Crimes of Color" inayozungumzia Maisha, Haki na Adha wanazokabiliana nazo jamii ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino).
Mkurugenzi wa Mafunzo na Elimu kwa Umma wa Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Rosemary Jairo akiwataka wanafunzi kutoa mapendekezo ni namna gani wataweza kusaidia kufikisha ujumbe kiurahisi kwa jamii kuhusiana na Haki za Binadamu ambapo pia amewataka wanafunzi wote waliohudhuria mafunzo hayo kuwa mabalozi katika kutetea haki za Binadamu kama zilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kwa kufikisha ujumbe kwa wenzao na katika jamii inayowazunguka.
Wanafunzi wakiwa wameshika Poster yenye Ujumbe maalum unaonyesha kwamba Binadamu wote ni sawa bila kujali aina ya Ulemavu mtu alionao.
No comments:
Post a Comment