Sunday, November 13, 2011

CHINA KUKUZA SEKTA YA UTALII NCHINI TAYARI UJUMBE WAKE WAJA KUANGALIA FURSA!

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi (mwenye miwani) akimkaribisha Makamu Gavana wa Jimbo la Jiangxi la China, Bw. Zhu Hong Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House tayali kwa majadiliano ya kusaini makubaliano ya mashirikiano ya kukuza sekta ya utalii nchini, leo asubuhi. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Utalii, Bi. Lilian Nyaki.Makamu Gavana wa Jimbo la Jiangxi la China akimkabidhi kitabu kinachoelezea vivutio vilivyopo jimboni mwake Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Ibrahim Mussa (wapili kulia) huku akishuhudiwa na Afisa Mkuu  wa Utalii na katibu mkuu.Ujumbe kutoka Jimbo la Jiangxi la China ukiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania mara baada ya kumaliza majadiliano ya jinsi pande hizo mbili zitakavyosaidia kukuza sekta ya utalii. Picha na Habari kwa Hisani ya Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Tulizo Kilaga, kilaga@mnrt.go.tz

No comments:

Post a Comment