Tuesday, November 8, 2011

SERIKALI YABUNI MPANGO WA KUHAMASISHA UTATUZI WA MIGOGORO YA KIKAZI KWA NJIA YA USULUHISHI!

Serikali imebuni mpango wa uelimishaji juu ya sheria za kazi kwa kuhamasisha utatuzi wa migogoro ya kikazi kwa njia ya usuluhishi na uamuzi kupitia tume ya Usuluhishi na uamuzi (CMA) ili kuwaongezea mahusiano kazini.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Wizara ya Kazi na Ajira yaliyoambatana na uzinduzi wa wiki ya hifadhi ya jamii yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam., Waziri wa Kazi na Ajira GAUDENSIA KABAKA amesema katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi tume hiyo imepunguza muda wa utatuzi kutoka wastani wa miaka mitatu na kufikia wastani wa siku 21 hadi 30.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Bi IRENE ISAKA anaeleza changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa wanachama wake.

No comments:

Post a Comment