Wednesday, November 2, 2011

AMREF YAKABIDHIWA VIFAA NA SONY ILI KULIWEZESHA KUTOA ELIMU YA MAAMBUKIZI YA VVU!

Shirika la afya na Utafiti AMREF Tanzania limekabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani laki moja na ishirini na kampuni ya SONY kwa lengo la kuliwezesha shirika hilo kutoa elimu kwa vijana na kuwahamasisha kupima afya zao.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Jijini Dar es salaam, Meneja Mpango wa AMREF, Dkt. AMOS MJIRENDA, amesema miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na Kampuni hiyo ni pamoja na Scrin yenye ukubwa wa nchi 150 ambavyo vinatarajiwa kutumika katika utekelezaji wa mradi unaofahamika kama Public viewing project katika kukabiliana na virusi vya ukimwi pamoja na mangojwa ya malaria na kifua kikuu.


Kwa upande wake Meneja mwandamizi Idara ya uwajibikaji wa kijamii, kutoka Kampuni ya Sony, ASAKO TOMURA, amesema wametoa vifaa hivyo kwa lengo la kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Mangonjwa hayo nchini.

No comments:

Post a Comment