Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeandaa vifaa vya kisasa vya kufanyia sensa kwa mwaka 2012 baada ya kukamilika kwa zoezi la sensa ya majaribio maeneo mblimbali nchini ambalo limeonyesha mafanikio.
Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu nchini Bi. REDEGUNDA MARO amesema katika zoezi hilo watatumia Scana ili kurahisisha kazi za uchapaji wa madodoso baada ya kujazwa ambapo mpaka sasa wanazo scana mbili zilizonunuliwa kwa ufadhiri wa shirika la UNFP na kuwa kwa mwaka 2012 watakodi Scana zipatazo 13 ili kurahisisha zoezi hilo.
Naye Kamisaa wa sensa ya majaribio Bwana PAUL KIMITI amesema sensa hiyo itafanyika kwa muda mfupi tofauti na miaka mingine iliyopita huku ikishirikisha vijana wengi zaidi kwa lengo la kuwafikia walengwa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment