Thursday, October 6, 2011

WAZIRI MKUU PINDA AZITAKA HALMASHAURI KUCHUKUA TAHADHARI YA MVUA ZA VULI ZINAZOTARAJIWA KUWA KUBWA!

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ameziagiza Halmashauri zote nchini kuchukua tahadhari ya madhara ya mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Octoba mwaka huu katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini.

Kupitia waraka wake aliousambaza katika halamshauri hizo kufuatia taarifa ya mwelekeo wa hali ya hewa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa mnamo Septemba 7 mwaka huu Waziri PINDA ametoa maelekezo ya kuchukua hatua za kujipanga kukabiliana na maafa endapo yatatokea.


Kufuatia hali hiyo tayari Halamshauri ya jiji la DSM kupitia afisa habari wake Bwana RAPHAEL KILAPILO amesema wataanza kutoa elimu ya afya juu ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu ,kuhara na malaria ambayo yanatokana na mafuriko na kuwaathiri hasa watu wanaoishi katika maeneo hatarishi.

No comments:

Post a Comment