Tuesday, October 25, 2011

WANANCHI WATAKIWA KUTOINGIZA ITIKADI ZA KIDINI KWENYE VYAMA VYA SIASA!

Wananchi wametakiwa kutoingiza misingi ya kidini katika vyama vya siasa ili kutoa nafasi kwa vyama hivyo kutetea maslahi ya wananchi, kulinda rasilimali za nchi na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi ili nchi iweze kupata maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Taasisi ya Islamic Peace Foundation SHEKHE SADIK GODIGODI amesema kuhusishwa kwa vyama vya siasa katika baadhi ya dini ni kutaka kudhoofisha nguvu ya vyama hivyo huku akionyesha hofu ya kuwepo kwa mkakati wa kudhoofisha vyama vyenye ushindani mkubwa.

No comments:

Post a Comment