Prof ANNE TIBAIJUKA UMEISIKIA HII?
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ilala Sharifu Shamba, Jijini Dar es salaam, wameulalamikia uongozi wa Serikali ya Mtaa huo kutokana na kujenga Ofisi za Serikali ya mtaa eneo la wazi na kusababisha adha kubwa kwa makazi yaliyoko pembeni mwa eneo hilo.
Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za kuzuia ujenzi huo usiendelee kutokana na kusababisha baadhi yao kushindwe kutumia eneo hilo bado uongozi wa mtaa huo umeendelea kukaidi na kuendelea na ujenzi huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bwana MTORO MAISHAA, amekiri kuwa eneo hilo ni sehemu ya wazi na kudai kuwa wanajenga baada ya kupewa notisi ya kuhama katika ofisi za awali walizokuwa wakitumia.
No comments:
Post a Comment