Monday, October 24, 2011
UN FAMILY DAY YAFANA KATIKA VIWANJA VYA LEADER'S CLUB.!
Mwishoni mwa wiki kulifanyika UN Family Day katika viwanja vya Leaders Club wakati wa Shamrashamra za wiki ya maadhimidho ya 66 ya Umoja Mataifa nchini ambapo ilipigwa mechi kati ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (White Jersey) na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (Blue Jersey) ambapo timu ya Wizara ya Mambo ya Nje iliibuka kidedea baada ya kuichapa timu ya UN bao 4-2.
Wazazi wakionekana kufurahi na watoto wao katika mkusanyiko huo uliokutanisha Familia za Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kucheza pamoja, kula pamoja, kunywa pamoja na kushiriki michezo mbalimbali.
Familia zikiwa pamoja.
Mgeni rasmi Mkuu wa Itifaki Balozi A. Itatiro akizungumza machache wakati wa UN Family Day na kusema kwamba siku hiyo haikuwa ya kusoma risala bali ni siku ya kufurahi pamoja....Happy Birthday UN..!!!
JAMANI NYIE VIPI JIPANGENI BASI TUANZE JUA KALI: Ililfika zamu ya Wakubwa kupimana nguvu katika mchezo wa kuvuta kamba baina ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.
Vuta nikuvute....!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment