Wednesday, October 12, 2011

MKAZI MMOJA WA RUVU AFA BAADA YA KUZIMIA MARA YA KUHUKUMIWA KIFUNGO!

Mkazi mmoja wa RUVU wilayani KIBAHA aitwaye IDDY ISMAIL,amepoteza fahamu kizimban wakati akisomewa mashtaka katika mahakama ya hakimu mkazi, na hatimaye kufariki dunia katika hospitali ya rufaa Tumbi alikopelekwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kamanda wa polisi mkoani PWANI ERNEST MANGU ,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, ambapo maerehemu alikuwa anshtakiwa kwa kosa la kuiba vifaaa tofauti vya shirika la reli.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya rufaa Tumbi, na uchunguzi juu ya sababu za kifo hiko unaendelea.

No comments:

Post a Comment