Madereva wa Taksi wa Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es salaam, wameulalamikia uongozi wa manispaa hiyo kufuatia kile walichosema kuwa umekuwa ukiwapatia kibali cha kufanya biashara hiyo katikati ya Jiji na kisha kuwageuka kwa kuwatumia Wakala wa MAJEMBE AUCTION MART kuwakamata na kuwatoza faini.
Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti baadhi ya Madereva wa Manispaa hiyo wamesema wamechoshwa na hali hiyo na kudai kuwa hawajui sababu ya wao kukamatwa huku wakiwa na vibali vyote vya kufanyia biashara katikati ya Jiji.
Aidha kwa upande wake Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala, Bi MARTHA MAINA, amekiri kuwepo kwa ushirikiano baina ya Manispaa na Wakala wa MAJEMBE AUCTION MART, kwa lengo la kukamata Taksi ambazo hazijasajiliwa na kudai kuwa wengi wa Madereva hao wamekuwa hawataki kusajiliwa nje ya mji na kusababisha msongamano katikati ya Jiji.
No comments:
Post a Comment