Baadhi ya Wananchi wakitembelea mabanda ya Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 Uhuru viwanja vya Mnazi Mmoja.
Waziri DK Shukuru Kawambwa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (Hawapo pichani)
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini wakiwa kwenye banda la Tume ya Vyuo Vikuu.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema ili kuboresha umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania imepanga kujenga shule za Sekondari za Kitaifa kote nchini ambazo zitatoa mchango katika kukuza kiwango cha elimu nchini.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi DK SHUKURU KAWAMBWA amesema ili kupanua wigo wa elimu ya Sekondari nchini, serikali itaboresha miundombinu ya shule hizo ikiwemo suala la maabara na upatikanaji wa vitabu vya kiada.
Kuhusiana na kuongezeka kwa idadi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika Waziri KAWAMBWA amesema hali hiyo inachangiwa na idadi kubwa ya watu wanaojiandikisha shule za msingi wanafunzi milioni 8.5 wako shuleni.
No comments:
Post a Comment