Sunday, September 18, 2011

MBUNGE WA PEMBA AKOSOA TAKWIMU YA SERIKALI YA WALIOKUWEMO KWENYE MV SPICE ISLANDER!

Takwimu iliyotolewa na serikali juu ya watu waliokuwa kwenye meli ya Spice Islander iliyopata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita, imekosolewa kuwa si sahihi kutokana na sensa ndogo iliyofanyika katika wilaya nne kisiwani Pemba, na kubainisha kuwa zaidi ya watu 2360 walikuwa kwenye chombo hicho.

Akitoa takwimu hizo jijini Dar es salaam leo Mbunge wa Ziwani Kisiwani Pemba Mh. AHMED NGWALI amesema ni idadi kubwa ya watu waliokuwa kwenye meli ya Spice Islander, kwani katika jimbo lake na maeneo jirani, kumebainika kuwa watu wengi hawajapatikana hadi sasa kutokana na ajali hiyo.


Aidha Mh Ngwali ameitaka serikali kuunda idara maalum itakayofanya uchunguzi wa kina, ili kuwafahamisha Watanzania idadi ya watu walikuwa kwenye chombo hicho, watu walioopolewa na waliokolewa katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment