Serikali imeombwa kushughulikia na kumaliza migogoro ya ardhi inayoikabili jamii nchini ili kupunguza vifo vinavyotokana na mapigano baina ya wamiliki halali wa maeneo na wavamizi.
Mmoja ya wajane Bi SOPHIA MNG’ONG’OSE mkazi wa Mlonganzila Wilayani Kisarawe mkoani Pwani ambaye mume wake alikufa baada ya kukatwa mapanga na mtu anayedaiwa kuvamia shamba lake, amewaomba watendaji wa serikali kukomesha migogoro hiyo kwa kuacha kugawa maeneo kwa zaidi ya mtu mmoja.
Bi SOPHIA alitoa ushuhuda huo kwenye tamasha la kumi la jinsia la siku nne linaloratibiwa na Mtandao wa Jinsia nchini TGNP na kushirikisha wanaharakati zaidi ya 5000.
No comments:
Post a Comment