Serikali imekiri kuongezeka kwa mapato kutokana na huduma zinazotolewa kupitia reli ya kati (TRL), baada ya kuondoka kwa wawekezaji wa kampuni ya RITES na uendeshwaji wa reli hiyo kubaki mikononi mwa wazalendo.
Akifungua Mkutano wa wadau wa usafirishaji nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa Wizara ya Uchukuzi, Naibu Waziri wa Uchukuzi Dokta OTHMAN MFUTAKAMBA amesema licha ya kuimarika kwa sekta ya usafirishaji nchini bado mchango wa wawekezaji unahitajika.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji Jijini Dar es Salaam SABRI MABRUCK ameitaka Serikali kuacha kutoa leseni za usafirishaji wa abiria kwa magari yanayobeba idadi ndogo ya abiria kwa lengo la kupunguza foleni za magari.
No comments:
Post a Comment