Wednesday, September 21, 2011

CHADEMA YAKATAA KULIOMBA RADHI BARAZA LA MAULAMAA KWA KUMVUA HIJABU BI FATMA KIMARO!

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimesema hakiwezi kuomba radhi kufuatia madai ya kudhalilishwa na kuvuliwa Hijabu kwa Mkuu wa wilaya ya Igunga FATMA KIMARO na wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa chama hicho, kutokana na suala hilo kuwepo mahakamani.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mshauri wa sheria wa CHADEMA Profesa ABDALAH SAFARI amesema wanasubiri ushahidi utakapothibitisha mahakamani ambapo amewataka Viongozi wa kiislam kuwa na subira badala ya kuwachonganisha waislam na chama hicho.

No comments:

Post a Comment