Wednesday, September 21, 2011

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOLEA UFAFANUZI SUALA LA KUDHALILISHWA MKUU WA WILAYA YA IGUNGA

                                                  FRANCIS KIWANGA (Kushoto)
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetolea ufafanuzi kuhusiana na kushindwa kutoa tamko kutokana na vitendo vya udhalilishwaji alivyofanyiwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga Bi. FATMA KIMARIO na wanaodaiwa kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Akizungumza na kituo hiki Mkurugenzi Mtendajiwa Kituo hicho FRANCIS KIWANGA amesema wakati wanajiandaa kutoa tamko kuhusiana na suala hilo hatua za kisheria zilichukuliwa ambapo watuhumiwa walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.


Katika hatua nyingine KIWANGA amesema tayari kituo chake kimepewa kibali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kupeleka waangalizi huru wa uchaguzi jimboni humo na watatoa ripoti kamili ya yaliyotokea baada ya kukamilika kwa mchakato huo.


Mbunge wa Viti Maalum kwa Tiketi ya CCM ZARINA MADABIDA tayari amekiomba Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA kuhakikisha kinamtetea Bi. FATMA KIMARIO kufuatia vitendo cha udhalilishaji alivyofanyiwa.

No comments:

Post a Comment