Baadhi ya CD bandia zilizokamatwa jana eneo la Mabibo mwisho na Msama Auction Mart.
Mmoja wa watuhumiwa wa uharamia wa kazi za wasanii akiwa kituo cha Polisi Urafiki jijini.
Mkurugenzi wa Msama Auction Mart akionesha baadhi za CD bandia alizozikamata eneo la Mabibo jijini DSM.
Wasanii nchini wametakiwa kuungana na kuwafichua maharamia wa kazi za sanaa waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kitendo kitakachosaidia kuutokomeza mtandao huo unaowanyonya na kuwafanya wasifaidike na matunda ya kazi zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kukamata CD bandia zenye thamani ya shilingi Milioni 18/- na mashine za kurudufu zenye thamani ya Milioni 5/- kwa wafanyabiashara BASHIR ABDUL na JOFREY ANATORI, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart ALEX MSAMA amesema kama wasanii wataungana wataishinda vita hiyo.
Hadi sasa tayari watuhumiwa wa uharamia wa kazi tofauti za wasanii kumi wameshakamatwa na nane wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi nchini wakati wawili miongoni mwao wakiwa nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment