Sunday, August 14, 2011

CUF KUMSIMAMISHA MGOMBEA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA IGUNGA!

                                                                 JULIUS MTATIRO
Chama cha Wananchi ( CUF), kimemtangaza rasmi Bwana, LEOPARD LUCAS MAHONA kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Igunga Mkoani Mara baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), ROSTAM AZIZ kujiuzuru hivi karibuni.



Akitanganza Jina la Mgombea huyo, Naibu katibu Mkuu wa CUF – Bara, JULIUS MTATIRO, amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na mgombea huyo kuwa mgombea pekee kutoka vyama vya upinzani nchini aliyewania jimbo hilo katika uchaguzi Mkuu uliopita dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, ROSTAM AZIZ .

No comments:

Post a Comment