Sunday, August 14, 2011

EWURA YAPANDISHA TENA BEI YA MAFUTA NCHINI!

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kwa mara nyingine bei mpya ya mafuta itakayoanza kutumika hii leo ambayo itahusisha Mafuta aina ya Petroli, Dizeli pamoja na mafuta ya taa.

Akizungumzia bei hiyo mpya, Meneja Biashara Mafuta wa EWURA, Mhandisi GODWIN SAMUEL, amesema kwa sasa bei elekezi kwa Petroli Jijini Dar es salaam itakuwa ni shilingi 2,114 kutoka 2,298, Dizeli shilingi 2031 kutoka 2213 huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa shilingi 2,005 kwa lita.

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa EWURA, TITUS KAGUO, amesema pamoja na Kampuni ya mafuta ya BP, kufungiwa kuuza mafuta ya petroli, dizeli na taa kwa miezi mitatu kampuni hiyo itaendelea kuuza mafuta mazito na yale ya ndege kutokana na kifungo hicho kutohusiha mafuta hayo.

No comments:

Post a Comment