Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii imeishauri Serikali kuanza kutatua migogoro ya mipaka iliyopo baina ya jamii na Hifadhi za Taifa ili kuleta maendeleo kupitia sekta hiyo.
Akiwasilisha mapendekezo ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Utalii JAMES LEMBELI amesema migogoro ya mipaka katika maeneo mengi inachangia kuongezeka kwa vitendo vya ujangili hali inayopelekea kuhatarisha usalama wa baadhi ya maeneo mengi nchini.
Katika hatua nyingine mwenyeikti huyo amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wananchi kusafirisha wanyama pori hai nje ya nchi na kuilalamikia Serikali kwa kutozingatia maoni na ushauri unaotolewa na wajumbe wa kamati hiyo.
No comments:
Post a Comment