Madereva TAXI katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam JNIA wameulalamikia uongozi wa eneo hilo kwa kuwapa eneo finyu ikilinganisha na idadi kubwa ya magari yao wanayoegesha kwenye eneo hilo.
Wakizungumza na kituo hiki madereva hao wamesema eneo wanalotumia lina uwezo wa kumudu magari 38 lakini mpaka sasa uongozi wa uwanja huo umetoa vibali vya kuegesha Taxi zisizopungua 160.
Kutokana na hilo Madereva hao pia wameutaka uongozi wa eneo hilo kuwarudishia eneo lao la awali. Theeastafrica ilipofuatilia suala hilo kwa uongozi ili kupata ufafanuzi haukufanikiwa baada ya Mkurugenzi mkuu wa JNIA kuwa kwenye kikao.
No comments:
Post a Comment