Ongezeko la watu na ujenzi holela jijini Dar es Salaam limetajwa kuchangia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushindwa kujenga barabara bora na zinazokidhi mahitaji ya wakazi wake kutokana na kupanda kwa gharama za fidia kwa watakaovunjiwa.
Akifungua maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam SAID MECK SADICK amesema katika maeneo mengi yanayotakiwa kuboreshwa wakazi wamegomea kuhama na wanapokubali gharama za kuwafidia huwa kubwa.
Kwa upande wake MESHACK ZADOCK Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja amesema kufanyika maonesho kama hayo kunawaongezea ufahamu wanafunzi kujua historia ya Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment