Wabunge mbalimbali walichangia hoja za wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, ambapo Mbunge wa Nyamagana(CHADEMA) Ezekia Wenje, amehoji juu yak watu wachache wanaojiona kuwa na haki ya kuishi katika maeneo yak pembezoni mwa fukwe mkoani Mwanza, huku wananchi walioishi maeneo hayo kwa miaka mingi wakiachwa bila fidia ya kutosha.
Aidha kufuatia matatizo ya ardhi ambayo yamekuwa yakiongezeka kila kukicha, amependekeza utaratibu utakaosaidia kutatua tatizo hilo hapa nchini.
Serikali imesema mpaka sasa haijaulipa Mfuko wa Hifadhi ya Jamiii(NSSF) kiasi chochote cha fedha, kwa kuwa mkataba uliosainiwa kati ya NSSF na serikali haujakamilika, hivyo mradi huo utakapokamilika ndipo malipo hayo yatakapoanza katika kipindi kisichozidi miaka kumi.
Naibu waziri wa Fedha Mh. GREGORY GEORGE TEU, ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa kondoa kusini JUMA SULEIMANI NKAMIA, aliyetaka kujua ni kiasi gani serikali imelilipa Shirika hilo toka lilivyoanza ujenzi wa Chuo kikuu cha Dodoma, kwani Tangu kuanza kwa ujenzi wa chuo hicho, shirika la NSSF ambalo linaendeshwa kwa michango ya wanachama wake pamoja na vitega uchumi walivyo navyo, limechangia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi.
No comments:
Post a Comment