Sunday, August 7, 2011

HIKI NDICHO ILICHOKIFANYA CHADEMA KWA MADIWANI WAKE WASALITI ARUSHA!

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imewavua uanachama madiwani wake watano wa jijini Arusha kwa madai ya utovu wa nidhamu na kutotekeleza maagizo ya kamati hiyo.Uamuzi huo umetokana na maazimio ya Kikao cha Kamati ya chama hicho kilichoketi mkoani Dodoma kwa muda wa siku mbili.


Kikukweli haya ni moja ya maamuzi ambayo kama chama kilihitaji kuchukua muda mrefu huko nyuma. Baada ya uongozi wa maonyo na kubembelezana chama lazima kiwe na uwezo kuchukua hatua. Siyo chama tu bali uongozi wowote uwe wa kazini au mahali popote huwezi kuongoza kwa maonyo na kuwabembeleza watu kuna wakati lazima uwe tayari kukata shauri.


Hili ndilo linalowashinda Chama cha Mapinduzi CCM katika kutekeleza azma yao ya kulivua gamba na kufikia kusogeza mbele maamuzi hayo kwa mwezi mmoja mbele.


Hivi karibuni Katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye alisema dhana ya mabadiliko ama kujivua gamba ni vema ikaeleweka kwa waandishi ili iwe rahisi kuwaeleza wananchi lengo hasa la dhana ya kujivua gamba, na kwamba Chama Cha Mapinduzi CCM kitaendelea kuisimamia serikali ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.


Ukweli unabaki palepale kwamba hakuna mtu ambaye anayeshindikana ndani ya chama hata kama uwepo wake umekipa chama sifa au kura kiasi Fulani. Hivyo uamuzi huu wa Chadema umewasha indiketa kwa CCM na viongozi wote ndani ya chama kuwa kuna wakati wa kubishana, kuzungumza na kujadiliana lakini pia kunawakati wa kukata malumbano.


Ilichokifanya Chadema imedhihirisha haiogopi kulipa gharama. Kwa mfano, ukija uchaguzi na chama hicho kikapoteza viti vyote vitano mtu anaweza akafikiria ni loss lakini kiukweli kabisa siyo loss kwao kwani kwa kuamua kuwatimua walishaamua kula loss ya kura, ruzuku na nafasi.

No comments:

Post a Comment