Sunday, August 14, 2011
IDARA YA SANAA NA SANAA ZA MAONYESHO UDSM KUADHIMISHA WIKI YA IDARA- FPA WEEK!
MNATANGAZIWA KUWA KUANZIA TAREHE 4, SEPTEMBA, 2011, IDARA YA SANAA NA SANAA ZA MAONYESHO YA CHUO KIKUU CHA DAR-ES-SALAAM ITADHIMISHA WIKI YA IDARA- FPA WEEK, KWA WIKI NZIMA.MAADHIMISHO HAYO NI UTARATIBU AMBAO IDARA IMEJIWEKEA KUANZIA MWAKA HUU NA YATAKUWA KILA MWAKA MWEZI WA NNE.
MWAKA HUU YAMESOGEZWA HADI SEPTEMBA KWA SABABU TU ZA KUUOANISHA NA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CHUO KIKUU CHA DAR-ES-SALAAM. MAADHIMISHO HAYA YATAHUSISHA KUONYESHA SHUGHULI ZA IDARA, NA MAONYESHO YA WADAU WAKIWEMO WANAFUNZI, NA WAHITIMU.
MNAKARIBISHWA KWA YAFUTAYO
I. KUSHIRIKI KATIKA MAFUNZO YA BURE YA WIKI NZIMA YA UANDISHI KWA AJILI YA FILAMU- SCRIPT WRITING. II. KUFANYA MAONYESHO YA KAZI ZAKO ZA SANAA UWE MWANAFUNZI AU MHITIMU III. KUSIKILIZA MADA MBALIMBALI ZITAKAZOTOLEWA IV. KUTOA MADA JUU ENEO LOLOTE LA SANAA V. KUPEANA UOZEFU WA MAISHA NA KAZI KAMA WASANII
KAMA UNA JAMBO LINALOHUSIANA UNATAKA KULIFANYA WAKATI HUO TAFADHALI TOA TAARIFA SASA HIVI NA ISIZIDI WIKI MOJA KABLA YA WIKI YENYEWE KUANZA, TAREHE 4 SEPTEMBA
WAKATI WA MAADHIMISHO YA FPA WEEK KUTAKUWA NA KUZINDULIWA KWA CHAMA CHA WAHITIMU WA IDARA - FPA ALUMNI ASSOCIATION. UZINDUZI HUU UTAANDAMANA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI- MWENYEKETI (MHITIMU), KATIBU (MWALIMU IDARANI), MWEKA HAZINA, NA WAJUMBE WA KAMATI KADRI YA KATIBA NA MAAMUZI YA WAJUMBE. WAHITIMU WOTE MNAKARIBISHWA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NA Charles Kayoka; ckayoka28@yahoo.com, au 0714429297/ 0786653712, 0766959349.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment