Sunday, August 14, 2011

NCCR-MAGEUZI CHAJITOA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA IGUNGA!

Chama cha NCCR – Mageuzi kimetangaza rasmi kujiondoa kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Igunga kwa madai ya kuzingatia maslahi ya vyama vya Upinzani nchini kwa kuunga mkono Mgombea atakayepitishwa kuwania nafasi hiyo katika Jimbo hilo.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Bwana SAMUEL RUHUZA, amevitaka vyama vya Upinzani nchini vilivyobaki kutafakari kwa kina njia muafaka kwa kumsimamisha mgombea mmoja ili kuhakikisha Jimbo hilo linachukuliwa na Chama kimojawapo cha upinzani.

No comments:

Post a Comment