Monday, August 15, 2011

AU YAITANGAZA AGOSTI 15 KUWA SIKU YA KUSAIDIA WALIOATHRIKA NA UKAME AFRIKA!

Umoja wa Afrika umetangaza rasmi Agost 15 kuwa ni siku ya kuungana na kuwasaidia watu milioni 12 ambao wameathirika na ukame, njaa na utapia mlo katika nchi zilizo katika pembe yak afrika, ambazo ni Somalia, Kenya kaskazini, na baadhi yak maeneo nchini Ethiopia.

Baadhi ya wasanii wa hapa nchini wanaungana kutoa sauti moja kuwahimiza waafrika kuunganisha nguvu zao katika kuwasaidia watu waliokumbwa na janga hilo.


Mwenyekiti wa umoja wa Afrika Dokta Jean Ping ametoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza kushiriki katika harambee hiyo, ambayo imebeba ujumbe usemao afrika moja, sauti moja kupinga njaa.


Agusti 25 mwaka huu wananchama wa umoja wa afrika watafanya mkutano mkubwa mjini Adis Ababa nchini Ethiopia kujadili namna yak kulitafuatia ufumbuzi tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment