Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limemaliza mradi wa ujenzi wa maghala 30 ya kikanda na ghala moja kuu ya kuhifadhi chakula nchini Uganda ili kutatua tatizo la upungufu wa chakula katika sehemu ya Afrika Mashariki inayokabiliwa na ukame.
Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema WFP itatoa mafunzo ya teknolojia ya uhifadhi wa mazao baada ya mavuno kwa wakulima elfu 25 wa Uganda.
Taarifa hiyo pia inasema maghala hayo yatawasaidia wakulima wadogo wadogo wa Uganda kuongeza uzalishaji wa chakula, ili kutatua tatizo la upungufu wa chakula la sehemu ya "Pembe ya Afrika" linalosababishwa na ukame.
No comments:
Post a Comment