Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mwamala kata ya Shirima wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuangalia upya upangaji wa bei ya mafuta kwa iliyopo sasa inawakandamiza kimaisha.
Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wamesema kwa sasa wanauziwa lita moja ya mafuta kwa shilingi 3,000/- kutoka bei ya awali ya shilingi 850 kwa lita.
Katika hatua nyingine baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Kilindi CCM, BEATRICE SHELUKINDO wameendelea kupinga bei hiyo mpya ya mafuta na kushauri fedha zilizokusanywa kifisadi zitumike kupunguza makali ya bei hiyo.
No comments:
Post a Comment