Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou akitoa hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya Mwaka 2011, ambapo amesema Ripoti hiyo inaonyesha jinsi ambavyo Uharibifu wa Mazingira unavyochochea kuwepo kwa matabaka ya watu kutokana na kuongeza athari kwa watu ambao tayari hawana unafuu wa kimaisha. Amesema jisni ambavyo matabaka yanayohusiana na hali ya maendeleo miongoni mwa Wanadamu yanavyozidisha uharibifu wa Mazingira.
Mshauri wa Masuala ya Kiuchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara (katikati) akiwasilisha Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2011 kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ESRF Dkt. Hoseana Lunogelo.
Mkurugenzi Mkuu wa ESRF Dkt. Hoseana Lunogelo akitoa tathmini yake kuhusiana na ripoti hiyo wakati wa kipindi cha majadiliano.
Wadau wa UN na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Dunia ya Mwaka 2011 ambapo ameelezea umuhimu wa kuwa na Ripoti kama hizo kwa kuwa zinatoa muelekeo halisi wa Maendeleo ya Dunia katika nyanja mbalimbali. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ESRF Dkt. Hoseana Lunogelo, Mshauri wa Masuala ya Kiuchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Maendeleo ya Dunia ya Mwaka 2011akisaidiwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Wawakilishi wa Balozi mbalimbali, wafanyakazi wa UN, pamoja na Viongozi wa Serikali katika uzinduzi huo.(Picha zote na www.dewjiblog.com).
No comments:
Post a Comment