Tuesday, July 19, 2011

MGOGORO WA KIBINADAMU WAIKUMBA PEMBE YA AFRIKA!

Nchi za eneo la Pembe ya Afrika zikiwemo Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan na Uganda zinakumbwa na tatizo la ukosefu wa chakula.

Tokea mwaka jana, ukame mkali ambao haujawahi kutokea katika miaka 60 iliyopita umekuwa ukilisumbua eneo hilo. Watu zaidi ya milioni 10 wanakabiliwa na tishio la njaa katika nchi za Kenya, Ethiopia na Somalia. Jumuiya ya kimataifa inajitahidi kuwasaidia watu hao, lakini mgogoro wa kibinadamu hauwezi kuepukika.


Dadaab, ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani iliyopo kaskazini mashariki mwa Kenya yenye eneo la kilomita 50 za mraba inashuhudia ongezeko la kasi mno la idadi ya watu barani Afrika, ambapo kila siku wakimbizi 1,300 kutoka Somalia wanafika kwenye kambi hiyo ili kupata vyakula, maji na dawa.


Kina mama hawa wawili wanawakilisha mamilioni ya wakimbizi wanawake waliofika katika kambi ya Dadaab kutoka Somalia, ambao walikumbwa na matatizo makubwa njiani.


Watu hao wenye ugonjwa wa utapiamlo wanaokabiliwa na ukosefu wa maji na chakula, wanapaswa kufanya jitahidi kubwa na kuwa na nia imara ili kufika kwenye kambi hiyo.


Mama mmoja mwenye watoto sita hakutaka motto hata mmoja abaki njiani wakati wakielekea katika kambi hiyo, kila mara aliwabeba watoto wawili, baada ya kutembea kwa muda aliwabeba wengine wawili, na hatimaye walifika katika kambi hiyo.


Kambi hiyo awali iliweza kuchukua watu elfu 90, lakini sasa wakimbizi laki 3.7 wanaishi kwenye kambi hiyo. mratibu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamuValerie Amos ametoa wito kwa mashirika mbalimbali kwenda Somalia kuwasaidia watu hao, kwani kambi hiyo inashindwa kupokea wakimbizi zaidi.

No comments:

Post a Comment