Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya Basi dogo aina ya Isuzu Journey lenye namba T 893 AXL waliyokuwa wakisafiria kutoka Kurasini kwenda Mbagala kuligonga tela la gari namba T 454 AKU kwenye makutano ya barabara za Mandela na Kilwa.
Akizungumzia Ajali hiyo mmoja wa Mashuhuda, ADAM CHAMITI, amesema ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa basi Dogo aina ya Isuzu kushindwa kushika breki kufuatia breki hizo kutofanyakazi ipasavyo na kusababisha gari hiyo kwenda kujibamiza kwenye tela la lori lililokuwa mbele yake.
Naye mmoja wa wakazi walionusurika katika ajali hiyo, HAMZA TOU, amesema walikuwa wakitokea kurasini kwenda Mbagala kwenye harusi na kwamba baadhi yao wameumia vibaya huku wengine wakipoteza fahamu.
No comments:
Post a Comment