Sunday, July 17, 2011
RUBADA KUJENGA KIWANDA CHA MIHOGO WILAYANI RUFIJI!
Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA, ALOYCE MASANJA (Kulia)
Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji RUBADA imepanga kujenga kiwanda cha mihogo Wilayani Rufiji kitakachokuwa na uwezo wa kukusanya malighafi ya tani milioni nane kwa mwaka.
Akizungumzia ujenzi huo Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA, ALOYCE MASANJA amesema lengo la unjezi wa kiwanda hicho ni kuongeza thamani ya zao la Mihogo kulifanya liwe na tija kwa wakulima nchini ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kujihusisha na kilimo cha zao hilo.
MASANJA Ameongeza kuwa katika mradi huo wanatarajia kuajiri zaidi vijana ambapo katika hatua za awali wameazimia kuajiri vijana miambili hususani waishio Wilayani humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment