Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imewaachia huru washitakiwa 31 katika kesi ya kuvua samaki bila kibali katika Bahari ya Hindi, eneo la Tanzania, iliyokuwa inawakabili raia 36 wa mataifa mbalimbali.
Pia, washitakiwa watano wameonekana wana kesi ya kujibu ambao ni Kapteni wa meli wahandisi wa meli ya Tawariq 1 na mawakala wawili.
Mahakama hiyo pia, ilimwamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, aandae utaratibu wa kuwarudisha washitakiwa hao na warudishiwe hati zao za kusafiria na mshitakiwa Jackson Toya ambaye hana hati ya kusafiria arudishwe nchini Kenya haraka iwezekanavyo.
Jaji wa mahakama hiyo, Augustine Mwarija alitoa uamuzi huo mahakamani hapo hii leo katika kesi iiyokuwa inawakabili washitakiwa 37. Machi nane mwaka 2009 katika ukanda wa bahari ya Hindi eneo la Tanzania Washitakiwa hao walikamatwa wakivua samaki kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment